Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Liverpool na Man United zapigana vikumbo kwa Wharton

Wharton

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Liverpool inajiandaa kujiunga na Manchester United na Real Madrid kaktika mbio za kumsajili kiungo wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, kwa pauni milioni 80 msimu wa joto. (Mirror)

Manchester United huenda ikamsajili mshambuliaji Jean-Philippe Mateta, 28, msimu wa joto baada ya uhamisho wa siku ya mwisho wa Mfaransa huyo kutoka Crystal Palace kwenda AC Milan kugongwa mwamba. (Mirror)

Klabu za AC Milan, Chelsea na Newcastle zinavutiwa na mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 26, kwa uhamisho wa bila malipo msimu wa joto, ingawa hivi majuzi amerejea Juventus kukamilisha tiba ya msili wa kiuno. (Football Italia)

Manchester United pia wanataka kuimarisha safu yao ya kati na wanapania kumpa nafasi hiyo kiungo wa klabu ya Newcastle na mchezaji wa kimataifa wa Italia Sandro Tonali, 25. (Metro)

Everton wako tayari kupokea ofa mpya kwa winga wa Uingereza Dwight McNeil, 26, baada uhamisho wake kwenda Crystal Palace ya siku ya mwisho ya kutibuka. (Football Insider)

Newcastle inatarajiwa kufufua tena mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Reims na raia wa Ivory Coast Patrick Zabi, 19, katika miezi ijayo. (The i - Usajili unahitajika)

Sando Tonali

Chanzo cha picha, Getty Images

Kipa wa Leeds United Mfaransa Illan Meslier, 25, anaweza kuondoka uwanja wa Elland Road, huku klabu ya Uturuki ya Besiktas ikifanya mazungumzo. (Team talk)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka, 30, ambaye mkataba wake na klabu ya Bayern Munich unamalizika msimu wa joto, yuko njiani kuelekea Arsenal kwa uhamisho wa bila malipo. (Bayern Insider)

West Ham inaweza kumfukuza kocha mkuu Nuno Espirito Santo bila kulipwa fidia ikiwa klabu hiyo itashushwa daraja . (Athletic - Usajili unahitajika)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi