Falme za Kiarabu
| Umoja wa Falme za Kiarabu الإمارات العربية المتحدة al-Imārāt al-‘Arabīyah al-Muttaḥidah | |
|---|---|
| Kaulimbiu: الله، الوطن، الرئيس ("Allah, Taifa, Rais") | |
| Wimbo wa taifa: Īshī Bilādī ("Uishi Nchi Yangu") | |
| Mji mkuu | Abu Dhabi |
| Mji mkubwa | Dubai |
| Lugha rasmi | Kiarabu |
| Lugha ya taifa | Kiarabu cha Kiemirati, Kiingereza |
| Mohamed bin Zayed Al Nahyan | |
| Mohammed bin Rashid Al Maktoum | |
Historia | |
• Mkataba wa ulinzi wa Uingereza (nchi za Trucial) | 1820 na 1892 |
• Uhuru kutoka Uingereza | 2 Desemba 1971 |
• Ras Al Khaimah yaungana | 10 Februari 1972 |
| Eneo | |
| • Jumla | km2 83,600 (ya 114) |
| Idadi ya watu | |
| • Kadirio la 2024 | 11,027,129 |
| • Msongamano | 132/km2 |
| PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
| • Jumla | ▲ $849.8 bilioni |
| • Kwa kila mtu | ▲ $77,251 |
| PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
| • Jumla | ▲ $545.1 bilioni (ya 26) |
| • Kwa kila mtu | ▲ $49,550 |
| HDI (2023) | ▲ 0.940 - juu sana |
| Gini (2018) | 26 |
| Sarafu | Dirham ya UAE (AED) |
| Majira ya saa | UTC+04:00 (GST) |
| Msimbo wa simu | +971 |
| Jina la kikoa | .ae .امارات |
Falme za Kiarabu, rasmi kama Umoja wa Falme za Kiarabu (kwa Kiarabu: الإمارات العربيّة المتّحدة; kwa Kiingereza United Arab Emirates) ni shirikisho la emirati au falme ndogo 7 katika kaskazini-mashariki ya Rasi ya Uarabuni kwenye mwambao wa ghuba ya Uajemi. Shirikisho limepakana na Saudia na Omani kwenye nchi kavu; baharini kuna mipaka pia na Katar na Iran. Mji mkuu ni Abu Dhabi na mji mkubwa ni Dubai.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Maeneo ya Falme za Kiarabu pamoja na Qatar na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao.
Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huu ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20.
Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi mwaka 1971, ambapo madola hayo madogo yalipata uhuru. Saba kati yake yaliungana kwa jina la Falme za Kiarabu.
Demografia
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2013, wakazi wote walifikia milioni 9.2; kati yao, 1.4 raia na 7.8 wahamiaji. Hivyo asilimia 85 za wakazi ni wageni, kumbe wenyeji ni sehemu ndogo tu. Zaidi ya nusu ya wageni wanatoka katika nchi za Bara Hindi.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarabu ambacho wenyeji wanakisema kwa lahaja maalumu ya Ghuba ya Uajemi. Tangu wakati wa ukoloni, Kiingereza kinatumika sana na kwa kawaida kinahitajika ili kupata kazi. Wahamiaji wanaendelea kutumia pia lugha zao za asili.
Uislamu ndio dini ya wenyeji (85% Wasuni na 15% Washia) na dini rasmi ya nchi, lakini kuna uhuru wa dini kwa wote, isipokuwa si uhuru wa kuieneza kwa wengine. Kati ya wakazi wote, Waislamu ni 76-77%, Wakristo (hasa Wakatoliki) ni 9-12%, Wahindu ni 4%, Wabuddha 2%, n.k.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Falme za Kiarabu zimekuwa nchi tajiri kutokana na akiba kubwa za mafuta ya petroli. Utajiri huo unapatikana kwa viwango tofautitofauti kati ya emirati zinazozunda shirikisho hili.
Abu Dhabi ni emirati mwanachama kubwa; ina pia kiasi kikubwa cha petroli na mapato makubwa kutokana na mauzo ya mafuta.
Emirati za Dubai na Sharjah zinazalisha pia petroli.
Emirati nyingine zinategemea msaada unaotolewa na Abu Dhabi hasa kutokana na mapato yake; pesa hizo zinasaidia ujenzi wa barabara na miundombinu kwa jumla.
Kazi nyingi za ofisini, viwandani, katika biashara na huduma zinatekelezwa na wageni ilhali wenyeji wanashika nafasi ya juu pekee; wengine wasio na vipaji vya kuongoza wanategemea malipo kutoka serikali.
Sheria ya nchi inasema ya kwamba makampuni yote nchini yanapaswa kuwa mikononi mwa raia wazalendo. Hali halisi inamaanisha ya kwamba wageni wanaunda kampuni wakimtafuta mwenyeji anayekubali sehemu ya mali na malipo ya kila mwaka bila kufanya kazi; lakini bila mwenyeji katika uongozi kampuni hairuhusiwi kuendesha shughuli zake kama ni kiwanda, duka au hoteli.
Makampuni kutoka nje yanaweza kupata leseni ya biashara kwa muda katika kanda za pekee bila kumshirikisha mwenyeji.

Falme za shirikisho hili ni:
| Jina | Eneo (km²) | Wakazi mwisho wa 2006 |
|---|---|---|
| Abu Dhabi | 67.340 | 2.563.212 |
| Umm al-Quwain | 777 | 68.000 |
| Fujairah | 1.165 | 130.000 |
| Ras al-Khaimah | 1.684 | 214.000 |
| Sharjah | 2.590 | 699.000 |
| Dubai | 3.885 | 1.327.000 |
| Ajmān | 259 | 258.000 |
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiarabu) (Kiingereza) Tovuti ya serikali Ilihifadhiwa 6 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine.
- (Kiingereza) UAEInteract.com Ilihifadhiwa 18 Septemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- United Arab Emirates entry at The World Factbook
- InterNet Website Services Provider IN UAE Ilihifadhiwa 5 Novemba 2014 kwenye Wayback Machine.
- Falme za Kiarabu katika Open Directory Project
- United Arab Emirates profile from the BBC News.
- United Arab Emirates country profile from the Lebanese Economy Forum, extracted from the CIA Factbook & Worldbank data.
- Wikimedia Atlas of United Arab Emirates
- World Bank Summary Trade Statistics United Arab Emirates
- Bohra caste relations
| Nchi na maeneo ya Asia |
|
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
| 1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Falme za Kiarabu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |